#50 Cent and Justin Bieber! ni topic inayojadiliwa zaidi sasa hivi kwenye mtandao wa twitter, kwanini?
Unakumbuka 50 alikuwa hampendi Justin na mpaka mwaka 2010 alimpa jina la "Justin Beaver" ? Okay, pambano la ndondi kati ya Floyd Mayweather na Miguel Cotto limewakutanisha.
50, Lil Wayne na Justin walikuwa wageni wa heshima walioalikwa na Floyd na walipata bahati ya kubeba mikanda ya Mayweather na kuwa ruhusa ya moja kwa moja ya kupanda ulingoni kumpongeza baada ya kuibuka mshindi.
Kukutana kwao ambako kumewavutia wengi kunaweza kuzaa kitu kizuri sana sio?
Mpaka leo Lil Wayne amekataa kufanya ngoma na Bieber pamoja na umaarufu wake. Kwa uzito wa kukutana kwao kwenye pambano hilo bila shaka mashabiki wao wote wangependa kuona kitu kama hiki: 50 Cent Featuring Justin Bieber and Lil Wayne! What a hit!


No comments:
Post a Comment