Saturday, May 12, 2012

Lady Jaydee na Piano siku hizi 'hawaachani'


Hakuna kitu kinachomuumiza msanii kama kuambiwa kuwa yeye si mwanamuziki kwakuwa hajui kupiga chombo chochote cha muziki.

Mbaya zaidi kama huo ndio ukweli.

Japo sio lazima kwa msanii kuwa na quality hizo, ni muhimu katika career yake na ni kitu anachoweza kujivunia.

Huenda ndo sababu hivi karibuni Lady Jaydee ameamua kuchukua mazoezi ya kutosha katika kifaa kimoja wapo muhimu katika muziki, Piano.

katika blog yake kunaonekana picha akiwa na mume wake Captain G wakifanya shopping kwenye duka la piano mjini Capetown, Afrika kusini la Allen & Fisher.

Ukifungua tu ukurasa wake wa twitter utakutana na picha ya piano kama background. Mambo mengine yanaendelea lakini kwa sasa ni kitu kimoja tu Jide angependa kusema "kwa kipindi hiki mazungumzo yangu ni Piano tu, mpaka hapo litakapotokea jingine jipya"


No comments:

Post a Comment