Kwa wengi jina la Cynthia Masasi halina uenyeji mzuri katika vichwa vyao. Lakini kwa wapekuzi wa muziki wa Hippop na video zake huenda wameshawahi kuiona sura yake lakini wasijue kama ni mtanzania.
Ameonekana kwenye video za wakali kama T.I, Juvenile, Jazze Pha, Rick Ross na wengine wengi na ukimuona hana tofauti sana na video vixen wengi wakali kama Maliah Michael ama Ambar Rose.
![]() |
| Cynthia na Rick Ross |
Ameonekana pia kwenye screen za silver kwa kuigiza kwenye movie binafsi kama Princess Zara and the Lover Boy in America, Paparazzi, This is Houston na Rebound.
![]() |
| Akiwa na Akon |
Ni mzaliwa wa Mwanza, na Mungu kamjalia urembo mtoto huyu! Akiwa Marekani ameonekana kwenye cover za magazeti makali na kumpa promo kubwa kama model kutoka Tanzania.
Pamoja na kuonekana kwenye video za ngoma kibao, Cynthia Masasi anaamini kuwa video nyingi za hiphop zinawadharirisha wanawake.
![]() |
| Hapa yupo na Trey Songz |
Pengine kauli hiyo inatokana na kuhisi umri wake unaenda na angehitaji naye pia kuitwa Mama na kuwa na familia.
Na ndo maana aliamua kurudi nyumbani Tanzania kuendelea na maisha ya kawaida kama Mama wa mtoto mmoja wa kiume wa miezi kadhaa na mume wake mfanyabiashara na tajiri kijana Richard Mziray.
![]() |
| Mziray na Cynthia kwenye mkoko wa hatari! |
Wapenzi hao vijana wameendelea kuvitikisa vichwa vya watu kwa kuishi maisha kama ya mbele na kumiliki ndinga za maana mjini huku zingine zikiwa na customized plate number.
![]() |
| Kitu cha Range kikiwa na customized plate number |
![]() |
| Clinic time |
![]() |
| Will you marry me? |
![]() |
| Mjengoni |
Ama hakika Cynthia Masasi na Richard Mziray wanakula bata la haja!










No comments:
Post a Comment