Jumatano ya May 23 mwaka huu kutafanyika Grand Finale ya American Idol season 11.
Mpaka sasa ni kama tayari watu wanamjua mshindi.
Kwa vyovyote vile kati ya Jessica Sanchez na Joshua Ledet mmoja ataibuka mshindi.
Jessica Sanchez amekuwa kipenzi cha wengi. Ni binti mwenye miaka 16 tu lakini sauti yake ni nzuri isiyo na kifani. Kuna wakati Jennifer Lopez ambaye ni judge katika mashindano hayo alisema haamini kama sauti hiyo tamu inatoka kwenye umbo la dogo la msichana huyo mwenye asili ya kifilipino.
Akon hakuficha mapenzi yake kwa binti huyu pale aliposhiriki kama mgeni katika mashindano hayo kwa kuwaelekeza masuala mbalimbali washiriki. Akon alisema anatamani Jessica Sanchez asishinde ili amchukue kwenye label yake.
Kwa upande wake Joshua, kila perfomance anayoifanya huwainua majaji. Ni kijana aliyekua kwa kuimba gospel lakini aliyeonesha uwezo wake mkubwa kwenye nyimbo za kawaida. Hata kama asiposhinda, Joshua atakuja kuwa staa mwenye mafanikio makubwa.
Katika show hiyo ya fainali Rihanna ataperform wimbo wake mpya “Where Have You Been” kutoka kwenye albam yake ya Talk That Talk ya mwaka huu pamoja na na mshindi wa Season Seven ya American Idol David Cook atakayeimba wimbo wake “The Last Song I’ll Write For You.”
No comments:
Post a Comment